Morrison Ashikiliwa na Polisi Kwa Madai ya Kujeruhi Shabiki



Mchezaji wa Simba, Bernard Morrison anashikiliwa katika kituo Cha Polisi Cha Chang’ombe jijini Dar es Salaam kwa madai ya kumjeruhi shabiki wa Yanga na kitu chenye ncha kali.

Wasafi Media imezungumza na Mkuu wa Kituo Cha Polisi Chang’ombe, ASP Mohammed Simba ambapo amethibitisha kupokea kesi hiyo “Ndio tumepokea hiyo kesi na tunaendelea na mahojiano tukikamilisha tutawajulisha,”

Tukio hilo limetoka mara baada ya Derby ya Kariakoo kutamatika katika uwanja wa Benjamin Mkapa hii leo.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post