Mfungwa wa Afrika Kusini Thabo Bester, ambaye pia anajulikana kama mbakaji wa Facebook kwa kutumia mtandao huo wa kijamii kuwarubuni wahasiriwa wake, amepatikana akiwa amefariki katika chumba chake cha gereza, kulingana na ripoti za vyombo vya habari nchini humo.
Msemaji wa Idara ya Huduma za Magereza (DCS) amenukuliwa akithibitisha kifo hicho katika jela la Mangaung huko Bloemfontein.
Singabakho Nxumalo alisema uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo cha kifo hicho.
"Aligunduliwa mwendo wa saa 03:35 hivi [Jumanne] asubuhi, ambapo seli yake iliteketezwa, alipatikana sakafuni," Bw Nxumalo alisema, kulingana na shirika la utangazaji la SABC.
Bester alikuwa akitumikia kifungo chake kwa mauaji ya mwanamitindo 2012.
Hapo awali alipatikana na hatia ya kubaka na kuwaibia wanamitindo wawili waliokuwa wamewavutia kwenye mtandao wa Facebook
Post a Comment