Mayele Atetemesha Mei Mosi Dodoma



Dodoma. Mtindo wa ushangiliaji wa mshabuliaji Yanga, Fiston Mayele umebamba katika kilele cha maadhimisho ya Sikukuu ya Wafanyakazi Dunia yanayofanyika katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Benki ya Muziki ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliibua shangwe kwa wananchi baada ya kutumbuiza huku wakicheza aina hiyo maarufu tetema.

Vijana waliokuwa wamekaa Jukwaa la upande wa pili walianza kushangilia kabla ya mashabiki kuanza kupiga kelele za shangwe wakiwaiga.

JKT walikuwa wanaimba wao wakitikisa mabega na kupeleka kichwa mbele hali iliyowafanya wanafunzi kuinuka na kuanza kuwaiga na watu wakaanza kushangilia.

Hata hivyo jana mchezaji huyo alishindwa kutetema baada ya timu yake kutoka suluhu ya bila kufungana walipocheza na watani zao Simba.

Kama Mayele angefunga jana katika mchezo dhidi ya watani huenda kelele zingekuwa za juu uwanjani hapo kutoka kwa mashabiki na wapenzi wa Yanga.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post