Manara Atoa Mpya "Hivi Kwelli Niliwahi Kuwa Simba Sipati Majibu"


Msemaji wa Klabu ya Yanga Haji Manara @hajismanara amesema hawezi kuwaacha Wapenzi, Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo kwakuwa wamempa heshima kubwa.

Manara amesema kuna wakati huwa anajiuliza kama kweli aliwahi kuwa katika Klabu ya Simba na kushindwa kupata majibu kutokana na upendo anaoupata kutoka kwa Mashabiki wa Yanga.

“Wananchi sitawaacha, hawa wamenipa heshima sana, Klabu hii ni Klabu ya Watu na wakati fulani siku hizi huwa najiuliza hivi Mimi niliwahi kuwa Simba? nilikuwaje! na nikimuona Mtu anashabikia Simba naona huyu aaaaaa!”

Manara yupo Mkoani Njombe kwa mwaliko wa Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa @kissagwakisakasongwa ili kutangaza utalii na shuguli mbalimbali zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika Wilaya hiyo.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post