Kocha wa Simba Pablo Akubali Yaishe Ligi Kuu Atoa Tamko Kuwa Yanga Bingwa-Michezoni leo

Kocha Mkuu wa Simba, Mhispania, Pablo Franco (kushoto). Kulia ni Kocha wa Yanga, Nesreddine Nabi.

 

KOCHA Mkuu wa Simba, Mhispania, Pablo Franco, amekubali yaishe baada ya kutamka kuwa watani wao wa jadi, Yanga tayari wameukaribia ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu na wana nafasi kubwa ya kuubeba.

 

Mhispania huyo ametoa kauli hiyo mara baada ya mchezo wa Kariakoo Dabi uliozikutanisha timu hizo uliochezwa wikiendi iliyopita Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam na kumalizika kwa matokeo ya 0-0.

 

Simba hivi sasa wapo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wakiwa na pointi 42, huku Yanga wapo kileleni wakiwa na pointi 55.

Kikosi cha timu ya Yanga.

Akizungumza na Spoti Xtra, Pablo alisema suluhu waliyoipata dhidi ya Yanga imewavurugia mipango ya ubingwa wa ligi msimu huu.

 

Pablo alisema walitakiwa kushinda mchezo huo, lakini matokeo hayo yana faida kwa Yanga ambao wamezidi kujiimarisha kileleni.

 

Aliongeza kuwa, ngumu kwao kuchukua ubingwa wa ligi na badala yake wanatakiwa kujipanga kwa ajili ya msimu ujao ili wawapoke taji hilo Yanga.

 

“Mchezo wetu dhidi ya Yanga ulikuwa wa mzani sawa, kiukweli ni matokeo mabaya kwetu, lakini mazuri kwa Yanga ambayo yana faida kubwa kwao.

 

“Kama kocha nikiri kuwa Yanga wanaukaribia ubingwa wa ligi na siyo sisi, hilo lipo wazi wapinzani wetu wametuacha kwa idadi nyingi ya pointi.

 

“Ili tuchukue ubingwa ni lazima Yanga ipoteze michezo mitano na sisi tushinde yote, kitu ambacho ni kigumu, licha ya katika soka lolote linaweza kutokea,” alisema Pablo.

Simba imeachwa pointi 13 na Yanga katika Ligi Kuu Bara msimu huu.

WILBERT MOLANDI

The post Kocha wa Simba Pablo Akubali Yaishe Ligi Kuu Atoa Tamko Kuwa Yanga Bingwa appeared first on Global Publishers.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post