Kauli ya Udhaifu wa Ligi Kuu ya Mpira Yamuibua Ally Mayay "Unajilinganisha na Nani?"



Mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga, Ally Mayay amefunga juu ya ubora wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kusema kuwa wanaosema kuwa Ligi hiyo ni dhaifu wanalinganisha na Ligi ipi. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mjadala wa ubora wa Ligi hiyo umeibuka hivi karibuni, kufuatia msemaji wa klabu ya Simba Ahmed Ally, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, kwa kuandika kuwa, Ligi ya msimu ina timu nyingi ambazo ni dhaifu hivyo bingwa anaweza kupatikana kwa kuwafunga wadhaifu.

“Timu nyingi Msimu huu zimekua dhaifu, tupo mzunguko wa 22 lakin ni timu tatu tu zimefikisha point 30, Msimu uliopita hadi kufika mzunguko wa 22, japo timu zilikua nyingi lakini timu 7 zilikua na points 30. Hii ni hatari kwa sababu Bingwa anaweza kupatikana kwa kufunga waidhaifu wengi.” Aliandika Ahmed

Taarifa hiyo ilipelekea kumtafuta mkongwe wa soka nchini ambae pia ni mchambuzi, Ally Mayay (Tembele) na kufafanua kuwa, kama Ligi yetu utataka kuifananisha na Ligi za barani Ulaya au Afrika ya Kaskazini basi lazima utaiona dhaifu, lakini kwa ukanda huu wa Afrika mashariki ni moja ya Ligi Bora.


“Lazima kwanza ujue unajilinganisha na nani, kama unalinganisha na timu za ulaya ni kweli dhaifu, na hata Afrika Kaskazini ni miongozni mwa Ligi zilizokuwa kwenye viwango bora.”

“Hatuwezi kusema dhaifu kwa ukanda wa Afrika Mashariki, sisi tupo juu ukiacha sudani kwa kuwa bado baadhi ya timu zao zinafanya vizuri.” Alisema mchambuzi huyo

Mpaka sasa Ligi Kuu Tanzania Bara imebakisha michezo nane kwa baadhi ya timu, huku klabu ya Yanga ikiwa kwenye kilele cha usukani wakiwa na 56, huku wakifutiwa na Simba kwenye nafasi ya pili wakiwa na pointi 43.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post