Mwimbaji nyota wa muziki wa RnB Bongo, Juma Jux amefunguka juu ya habari za chini chini kuhusu kurudiana na aliyekuwa mpenzi wake, mrembo Jack Clif akisema hajawahi kuonana na mrembo huyo tangu atokea jela na kurejea nchini.
Akizungumza leo kwenye The Switch ya Wasafi FM, Jux amesema wamewahi kuwasiliana mara moja na hakuna mahusiano ya kimapenzi kati yao kwani tayari ana mtu wake.
"Niwe muwazi hatuna mawasiliano yoyote lakini mara ya kwanza kabisa wakati ametoka tulishawahi kuwasiliana, alinitumia tu meseji basi tukaongea" amesema Juma Jux na kuongeza, "Kwa hiyo sasa hivi nadhani kitu kizuri ametoka ana uhuru wake kama kawaida hicho ndio kitu muhimu, mimi na maisha yangu, lakini kiukweli hatuna mahusiano yoyote."
Ikumbukwe, kabla ya Vanessa Mdee, Jux alikuwa kwenye mahusiano na mrembo huyo Jackie Cliff kabla ya kupata matatizo yaliyompelekea kufungwa kwa takribani miaka saba huko China.
Post a Comment