Hoteli Tatu za Tanzania Zaingia 10 Bora Afrika



RIPOTI ya Utajiri wa Afrika mwaka 2022 imezitaja hoteli mbili za Kampuni ya Grumeti Reserves kuwa miongoni mwa hoteli 10 bora zaidi barani Afrika.

Hoteli hizo ni Sabora Tented Camp na Mara River Tented Camp. Hoteli nyingine kutoka Tanzania iliyoingia kwenye orodha ya 10 bora Afrika mwaka huu ni Beyond Klein’s Camp.

Aidha, katika Afrika Mashariki, hoteli zilizotajwa katika orodha hiyo ya kumi bora ni Cotta’s 1920s Camp na Beyond Bateleur Camp za nchi jirani ya Kenya, pamoja na Sanctuary Gorilla Forest ya Uganda.

Hoteli nyingine nne zinazokamilisha idadi ya 10 Bora Afrika ni kutoka Botswana na Afrika Kusini.

Vigezo vilivyotumika kuzipa hoteli hizo viwango vya juu ni pamoja na ubora wa huduma, eneo zilipo, muonekano na mandhari, uhalisia wa mbugani na uwepo wa viumbe hai, wakiwemo ndege na wanyamapori.

Ripoti hiyo ya utajiri wa Afrika imekuja wakati ambao Tanzania imezindua rasmi filamu ya The Royal Tour inayotangaza vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji zilizopo nchini.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post