Pole kwake Majeruhi na Insha'Allah atakaa sawa soon, kwangu naona haikukaa sawa lakini tutasubiri taarifa ya Polisi rasmi, but na katika hili cc Washabiki pia kuna vitu tuendelee kuviepuka.
Nowadays sio ajabu kukuta Mtu anakutukana humu mitandaoni , matusi makubwa bila sababu,,ukienda katika profile yake kaweka hadi namba yake ya simu,,imagine ukimpata huyo mtu.
But haiondoi ukweli kujichukulia sheria mkononi ni kosa, all in all ,Yanga haiwezi kulichukulia hili jambo kishabiki kisa kafanya mchezaji wao, najua angefanya wa kwetu ,,mida hii tungekuwa tunaongea mengine hapa
Morrison (@bm3gh) ni mchezaji bora sana na pamoja na yote yalitokea baina yetu, tunaendelea kumpa respect kama Binadamu,,na tunaamini atatumia hekma zake kuweka sawa hili jambo.
Wananchi wenzangu, naomba mjadala wa hili jambo tuufunge na tuache Mamlaka sahihi zitatujulisha.
Katika Dunia ya Ustaarabu ni wajibu wetu kutokuwa na jazba ktk vitu kama hivi, Soka ni Mchezo wa kiungwana ndani na nje ya Uwanja, tunao wajibu wa kuheshimiana bila kugombana wala kutukanana matusi yanayoweza kumpanikisha mwenzio,
lakini pia Morrison mimi binafsi nakupenda uwezo wako wa uwanjani, Punguza hasira dogo,,Washabiki tuwazoee , mwenzio kutwa natukanwa humu na sijawahi kumshtaki au kuchukua hatua yoyote ile hata siku moja,,na nilitaka kumpata mmoja wapo,,ni nusu dakika tu.
Hata wewe uliwahi kuntukania hadi Mama yangu Mzazi humu humu Instagram ,lakini nikakusamehe coz sijui kesho yangu, nilijua uliaminishwa vitu vya uongo na ukasahau uhusiano wetu wa awali, yashapita kwangu na wewe nakuona best player miongoni mwa walio bora katika ligi yetu.
Ombi langu kwenu Washabiki wa Soka, tuendelee kutaniana bila kutukanana na tusamehe pale tunapokoseana, Nani aijuae kesho yake?
Na kuhusu Majeruhi naendelea kumtafuta ili tuweze kumsapoti ktk matibabu yake na Insha'Allah atakaa sawa na hili jambo litaisha kwa amani. 🙏
Cc @hajismanara
Post a Comment