MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Borussia Dortmund raia wa Norway Erling Braut Haaland amefuzu vipimo vya afya tayari kujiunga na klabu Ligi Kuu ya Uingereza Manchester City.
Haaland amefanyiwa vipimo hivyo nchini Ubelgiji na kwa mujibu wa taarifa ni kwamba mshambuliaji huyo tayari amesharejea kwenye kikosi cha Dortmund.
Taarifa zinasema Manchester City waliitaarifu Dortmund kuwa wapo tayari kutoa kiasi cha Euro Milioni 60 na siyo 75 ambazo ndiyo zinatakiwa kwa ajili ya kuvunja mkataba wake.
Mkataba wa mshambuliaji huyo unamruhusu kuondoka klabuni hapo kwa kiasi cha Euro Milioni 75 la sivyo ataondoka bure mwisho wa msimu ujao.
Haaland anatarajiwa kupokea mshahara wa Paundi 375,000 kwa wiki ambayo ni sawa na Bilioni moja na milioni Sabini na Nne Laki Nane Arobaini na Mbili Elfu na Mia Mbili Sitini na Nane (1074842268) pesa taslimu ya Kitanzania.
The post Haaland Afuzu Vipimo vya Afya Kujiunga na Manchester City Msimu Ujao appeared first on Global Publishers.
Post a Comment