Sanura Kassim almaarufu Bi Sandra au Mama Dangote; ni mama mzazi wa staa mkubwa wa muziki barani Afrika, Diamond Platnumz ambaye amejikuta akicharuka na kulipuka baada ya kuulizwa juu ya ujio wa mzazi mwenza wa mwanawe huyo, Zarinah Hassan au Zari The Boss Lady ambaye ametua Bongo wikiendi iliyopita bila kukanyaga kwa mama huyo.
Zari alitua Bongo akitokea nchini Afrika Afrika Kusini, lakini hakutoka nje ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar, badala yake aliunganisha ndege na kwenda kutua jijini Mwanza kabla ya kesho yake kuonekana akijiachia kwenye kiwanja cha bata cha Beach-Kidimwi jijini Dar.
Akiwa jijini Mwanza, Zari alifanya shughuli zake za kijamii kama kawaida yake akiwa ni balozi wa bidhaa za taulo za kike.
ZARI ASHAMBULIWA
Ujio huo wa Zari ulidaiwa kuibua makasiriko kwa baadhi ya Wabongo ambao walihoji kitendo cha mwanamama huyo kutua Bongo na kushindwa kufika nyumbani kwa kwa Diamond Platnumz, Mbezi-Beach au kwa Mama Dangote kule Madale ilihali aliweza kwenda kujiachia Kidimbwi.
Zari amejikuta akishambuliwa kwa kujiita wifi na shemeji wa Watanzania, lakini akashindwa kufika nyumbani kwa Diamond na wakwe zake kuwajulia hali hivyo kuhojiwa huo uwifi na ushemeji wa aina gani?
Sanura Kassim almaarufu Bi Sandra au Mama Dangote.
Hata hivyo, wengine walikwenda mbali zaidi na kusema kuwa, Zari alikuwa wifi na shemeji kipindi kile akiwa na Diamond na siyo sasa ambapo kila mmoja amechukua hamsini zake na si lazima kila akitua Bongo, basi aende nyumbani kwa jamaa huyo au kwa Mama Dangote.
MAMA DANGOTE ALIPUKA
Baada ya sakata hilo kugeuka mjadala wa kitaifa, Gazeti la IJUMAA lilimtafuta Mama Dangote ambapo baada ya kuulizwa kuhusu ishu hiyo aliwaka ile mbaya;
“Kwani kila akija lazima niwatangazie? Wao wanataka wafahamu kama nani? Kwani akija huwa ninawapa taarifa kwamba amekuja? Hao wanahoji ni kama nani? Ninyi andikeni mnavyotaka kuandika,” anasema Mama Dangote kwa hasira.
ZARI AJIBU MAPIGO
Kwa upande wake, mwanamama Zari ameibuka kuhusiana na wanahoji juu ya ishu hiyo na kujibu mapigo kwa kuwapa za chembe wale wote wanaomfuatilia yeye na maisha yake.
Zari anasema; “Unajua Watanzania wengine mimi siwaelewagi, nisipoenda Madale (nyumbani kwa Mama Dangote) au Mbezi (nyumbani kwa Diamond) wanasema ooh hawamtaki, hawaotaki kuonana naye.
“Nikienda wanasema Zari anapenda sana kuiganda na kujipendekeza kwenye hiyo familia.
“Nikienda wanaongea, nisipoenda wanaongea, sasa mtu afanye nini?
“Mimi hao watu (familia ya Diamond) ninaongea nao, nimefika nikawaambia hivi na hivi nimekuja kikazi, wakasema sawa Mama Tee enjoy.
“Sasa wewe unaumwa eti Zari hajaonana na Mama Dangote, kwa nini? Zari hajaonana na ile familia, kwa nini? Wewe unafaidika nini mimi nikionekana na Mama Dangote au mnataka nipigepige picha nirushe kwenye Instagram?
“Mimi siishi maisha ya Instagram. Inaweza kuonekana ni hivyo, lakini siyo hivyo, so I’m sorry (samahanini) mmekuwa disappointed (nimevunjika moyo), lakini ndiyo hivyo,” anasema Zari naye akiwa amepaniki ile mbaya.
ZARI NA WABONGO
Kwa muda mrefu, Zari amekuwa akirushiana maneno na baadhi ya Wabongo ambao kwa mujibu wake, wana makasiriko kutokana na kuzaa na Diamond kisha akaachana naye hukuakiwa vizuri kimaisha.
Hata hivyo, pamoja na hayo yote, Zari anasema; “Ni Kweli nimeachana na Diamond, lakini ninaipenda Tanzania…”
Stori; Khadija Bakari, Dar
Post a Comment