Diva Loveness Aguswa na Mrembo Aliyeuawa Mwanza Kwa Risasi Saba na Mumewe

Diva Ameandika haya


" Very sad , Huyu Dada @iam_swallher ameuliwa Usiku wa Kuamkia Jumapili Na Mume Wake anaeitwa Said kwa Kupigwa Risasi 7 Kichwani na kufariki hapohapo, alikuwa Maarufu Kwa Mkoa wa Mwanza kwa urembo wake lakini Pia alikuwa Make Up artist Maarufu Jijini humo, Kisa Cha Kufikia Mauaji hayo inadaiwa ni wivu wa Kimapenzi,
Mwanaume baada Ya Kufanya mauaji hayo alikimbia na mpaka dakika hii hajulikani alipo, ingawa kuna tetesi zinasema nae amejipiga risasi na haijiadhihirishwa kama ni kweli ila wasifu wake ni inasemekana ni mfanya biashara maarufu na anaejiweza kifedha na mara kadhaa alikuwa akimpiga dada huyu na kumtishia kuwa kuna siku angemiminia kichwani risasi , wazazi walihusika kuwasuluhisha na mara kwa mara alivumilia na kurudi kwa Mume wake, kuna siku alipigwa na kitako cha bunduki na kuzimia Masaa matatu mazima.
Mwenyezi Mungu amuweke Mahali Pema Amina!.
wanawake wenzangu Pls say NO to Violence ..
ondoka kabisa .. anaekupenda ata awe amekuoa kama anakupenda toka Moyoni hawezi kukurushia ata kibao , hawezi kukunyanyasa na hawezi kukupiga!.
ukatili wa majumbani umekuwa mkubwa sana na vyombo husika huchukulia kawaida suala hili, wazazi nyie pia ni chanzo kikubwa kwa kusema ndoa inahitaji uvumilivu au mtu akipingwa ndio Mapenzi rudi kwa mumeo mbona baba yako tunavumiliana Jaman kuna talaka iwapo mtashindwana iliwekwa sababu ya kuepuka vitu kama hizi, Huyo Mwanaume amezima ndoto za dada wa watu , Kama Wewe ni Mwanamke na una face hii hali Pls file a Report usije fikwa na umauti hakuna Mapenzi Ya Kupigana ,
Nawaombea wote mnaopitia Manyanyaso kusema Hapana kwa ukatili huu ,
Hii Haikubaliki kabisa .. naandika nikiwa najisikia vibaya sana kwa kuondokewa na moja kati Ya Followers wangu. Mwanamke Mwenzangu na Mtanzania Mwenzangu, Pole ndugu na Jamaa kwa msiba huu.

Pumzika Kwa amani Mpendwa!.
RIP beautiful"


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post