DIAMOND Platnumz Katika Vita Nzito Nyingine na Burnaboy na Wizkid


DIAMOND Platnumz au Simba; ni supastaa wa muziki nchini Tanzania ambaye kwa mara nyingine ameingia vitani na wasanii wakubwa barani Afrika wakiwemo Burna Boy, Wizkid, Davido na wengine.

Hii ni baada ya kutajwa kuwania tuzo kwenye kipengele kimoja huko nchini Ghana zinazokwenda kwa jina la Ghana Entertainment Awards USA (GEAWARDSUSA).
Majina ya wanaowania tuzo hizo yalitangazwa Mei 13, 2022 ambapo hadi sasa Diamond anashindania kipengele kimoja kwenye tuzo hizo.

Katika tuzo hizo kwenye msimu wake huu wa nne, Diamond anashindania Kipengele cha Best African Entertainer ambacho ni maalum kwa wasanii wote barani Afrika.
Mastaa wengine wanaowania kipengele hicho ni Davido, Wizkid, Burna Boy, Tems, Focalistic, Nasty Blaq, Pearl Thusi, Oduma Essan, Funke Akindele, Sydney Talker na Broda Shaggi.

Tuzo hizo kwa mwaka huu zitafanyika kwa mara ya nne na zinatarajiwa kutolewa Julai 8, 2022 huko jijini New York, Marekani.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post