Ujana, mapenzi na ustaa.
Maneno hayo machache yanatosha kuelezea maisha ya Wema Sepetu na Diamond Platnumz. Kama hukufaidi drama za hawa wawili, bado hujalijua vizuri game la muziki wa kizazi kipya.
Kwa ufupi sana, hii ndiyo couple namba mbili iliyokuwa na nguvu kuliko zote katika historia ya tasnia hiyo pendwa Tanzania. Couple inayoendelea kushikilia namba moja ni Ile ya Juma Nature na Sintah.
Tofauti na Nature aliyemuimbia Sintah nyimbo za hasira zisizozidi 3, Diamond yeye alitengeneza nyimbo nyingi za nyakati zote; chungu, tamu na chachu.
Nyimbo zenyewe:
1. Kizazizai
2. Moyo wangu
3. Nimpende nani
4. Nataka Kulewa
5. Nitampata wapi
6. Chanda chema
7. Mdogomdogo
8. Number One
9. Ukimuona
10. Mawazo
Kwa haraka haraka, nyimbo hizo ambazo zote zilihit zilimlenga Wema Sepetu kwa namna moja ama nyingine. Kazi kwenu wachambuzi kuzidadavua na ikibidi kurekebisha, kujazia au kupunguza.
By Interest
Post a Comment