Burna Boy na Davido Hapatoshi Huku NIGERIA Baada ya Kuachia Nyimbo Siku Moja

 


Mei 13 ukiachana na headlines za msanii @kendricklamar kudropisha Albamu yake ya Molare & The Steppers na mitandao kama Apple Music na Spotify kucrash kutokana na uwingi wa watu kuistream albamu hiyo, Back to Africa ambapo tarehe hii pia, @davido pamoja na @burnaboygram wapo kwenye macho ya mashabiki kuona nani atamgalagaza mwenzie kwenye projects zao ambazo wameachia pamoja, Davido akiwa na Stand Strong na Burna Boy akiwa na Last Last.


Masaa kadhaa nyuma, Davido alifanikiwa kushika No. 1 kwenye Apple Music Nigeria (Top songs) kitendo kilicho fanya aweke Insta story kuwa anaitwa 001,ishu ambayo kwa mashabiki imeonekana kama ni kijembe kwa Burna Boy ambaye alikuwa No.3, (sasa No. 2).


Mitandaoni Mashabiki wa Burna Boy na Wizkid wanaamini ni suala la muda tu, Burna Boy anaenda kuichukua No.1



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post