Tukio la bondia Mike Tyson Aprili 20 mwaka huu la kumchapa ngumi kadhaa za uso abiria mwenzake mmoja wakiwa kwenye ndege ya JetBlue baada ya kumchokoza kwa kumtolea maneno yasiyofaa, Mwanasheria wake amefunguka kuwa Tyson hana kesi ya kujibu. Kwa mujibu wa TMZ.
Mwanasheria huyo wa Mike Tyson, Bw Stephen Wagstaffe amesema Tyson hana kesi ya kujibu kwakua kijana aliyepigwa hajataka kufungua mashtaka yoyote na wote wamekubaliana kuyamaliza nje ya mahakama.
Haya yanajiri baada ya mashahidi kutoa ushuhuda kuhusu tukio hilo, ambapo kijana huyo aliyepigwa alionekana mwenye makosa zaidi kwakuwa alikuwa akimsumbua kwenye ndege bondia Mike Tyson.
Post a Comment