Benard Morison "Msinipigie Tena Simu Mtaaribu Simu yangu"



Mchezaji kiungo kutokea Klabu ya Simba Benard Morisson amewaomba mashabiki zake kuacha kumpgia simu kwani anahisi simu yake itapasuka😂

Kupitia ukurasa wake wa instagram Morisson ameandika
“Naheshimu sana upendo mlionionyesha, sichukulii poa hata kidogo.
Niliwaomba mnitumie Elfu moja lakini sasa simu na meseji ninazozipokea zinaenda kuuwa simu yangu, Birthday imeisha sasa naomba msinipigie tena, Mkiharibu simu yangu nitarudi hapa kuomba simu mpya.
Asante kwa aliyenipigia na kunitumia meseji NAWAPENDA PIA.” - @bm3gh

Siku ya kumbukizi ya kuzaliwa kwake (Mei, 20) Morisson aliwaambia mashabiki zake wamtumie Elfu moja kwenye namba yake kama zawadi kwa ajili ya birthday yake.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post