Beka Flavor Athibitisha Kuachana na Mama Mtoto Wake "Tunalea Mtoto Wetu Kama Wazazi"


Licha ya kuonekana nyuso zao zikiwa zenye bashasha kwenye usiku wa Listening Party ya FIRST BORN ALBUM ijumaa ya tarehe 20 mwezi huu, msanii Beka Flavour amekana kurudiana na Mama mtoto wake, Happy Reuter na kudai kila mmoja ana maisha yake na wao hukutanishwa na mtoto wao tu kama wazazi. Haya ameyaongea Beka Flavour akiwa kwenye Empire ya EFM, hii Leo Mei 23.

Beka na mzazi mwenzie waliachana sababu kubwa zikiwa ni wivu wa kimapenzi na kutoheshimiana baada ya Happy kufanya kazi ya Uvixen kwenye music video ya Ibraah toka Konde Gang ingali kazi yake ilikuwa ni kufanya Makeup pekee.

Beka akimtuhumu Happy kutomuheshimu na kujihusisha na uvixen bila kumtaarifu,huku Happy akiamini kinacho msumbua Beka ni wivu uliopitiliza.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post