Ikitajwa orodha ya wasanii chipukizi kwenye tasnia ya muziki wa Bongo fleva wanaolivutia kundi kubwa la wadau na mashabiki wa muziki huo, basi huwezi kuliacha jina la mwanamuziki Hanstone kijana aliyerithi mikoba ya talanta ya muziki kutoka kwa Marehemu baba yake mzazi mwanamuziki Banza Stone ‘Mwana Masanja’.
Miezi kadhaa iliyopita matarajio ya wengi yalikuwa ni kumuona kinda huyo akitambulishwa kama msanii mpya wa record Label maarufu Afrika mashariki ‘WCB Wasafi’ chini ya msanii Diamond Platnumz, jambo ambalo halikuwezekana kutokana na sababu kadhaa ikiwamo kile kilichotajwa kuwa ni kukosekana kwa maelewano ya kikazi kati yake na uongozi wa Label hiyo.
Jambo hilo lilipelekea msanii huyo kujiengua na kuendelea na harakati za muziki wake yeye binafsi.
Baada ya kimya cha muda mrefu, hatimaye Hanstone ameibuka na kuzua mjadaa unaoenea chini kwa chini kuhusu uhusiano wake na mwanamuziki Harmonize, punde baada ya kuweka ujumbe mfupi kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram unaoashiria uwepo wa ukaribu baina yake na Konde Boy.
”I love you bro Harmonize” unasomeka ujumbe huo alioundika Hanstone.
Huku maswali ya wengi ni Je, Pengine Harmonize akamsaini Hanstone kwenye record Label yake baada ya kuondoka chini ya Wcb au nini kinaendelea baina yao hata kupelekea mwanamuziki huyo kuweka bayana kiwango cha upendo wake kwa msanii Harmonize ?.
Ikumbukwe punde baada ya Hanstone kujiengua na kuanza kufanya shughuli zake za muziki akiwa mwenyewe, mnamo Oktoba 2021 alifanikiwa kutoa Extended Playlist yake iitwayo “Amaizing” yenye jumla ya nyimbo sita zilizofanikiwa kufanya vizuri.
Aidha licha ya kuwepo kwa mijadala mbali mbali kuhusu kilichovuruga uhusiano wa msanii huyo na uongozi wa WCB, bado hakuna upande wowote ulieleza kwa undani kuhusu suala hilo.
Post a Comment