1: MECHI 3 BILA USHINDI. MECHI 3 BILA BAO. Sumu kubwa inayootesa Yanga kwa sasa ni kukosa 'CHAMPION MENTALITY'. Hofu ni kubwa sana kwenye vifua vya Viongozi, Benchi la Ufundi na Wachezaji. Ni kama Yanga wanacheza wakiwaza zaidi 'Gap' ya Pointi kuliko Dakika 90 za mchezo husika
2: Sumu nyingine inayowatesa Yanga ni MAYELE. 'Ushabiki' wa jukwaani umehamia uwanjani. Ni kama Yanga wamesahau kuwa jambo muhimu zaidi ni YANGA KUSHINDA sio MAYELE KUTETEMA
3: Kipindi cha pili Prison walirudi vyema kwenye 'Low Block' na kupunguza hatari tofauti na ilivyokuwa kipindi cha kwanza. Jambo pekee ambalo kocha wa Prison anatakiwa kulifanyia kazi ni kujua namna gani Timu yake inacheza ikiwa na mpira. Ni aibu kwa Timu ya Ligi kuu kuwa 'Poor' kiasi kile kwenye Positive Transition. Kwanini?
4: Yanga walicheza kwa presha sana. Muda waliosukuma watu wengi mbele, Safu yao ya ulinzi ilikuwa imevurugika kwenye mpangilio wao. Ilikuwa nafasi nzuri kwa Prison kutega 'counter Attack na kuwaadhibu Yanga
5: Well Done Golikipa wa Prison, Hussein Abel 👏 Ni nyota wa mchezo kwa upande wangu. Sahau kuhusu 'Saves' rudi na utazame jinsi alivyokuwa anaipanga safu yake ya ulinzi kudili na krosi za Yanga..
6: 'Sub' ya Makambo ilikuwa sahihi, kilichokosea ni mtu aliyetoka. Sure Boy alikuwa Plan B ya Yanga kwenye kupita katikati. Kumtoa kuliiacha Yanga na mpango wa krosi tu. Kitu ambacho walishaonekana kufeli kuanzia mwanzo
7: Jumanne Elfadhil.. 👏 What A Warrior! Mtu haswa. Alijitoa sana kwenye kugombea mipira ya 50/50 na akawa msaada kwa kudumbukia katikati ya Chona na Mwihambi kwenye kucheza krosi
8: Mliodhani shida ni Cedric Kaze pekee, Leo mmepata majibu. Shida ni benchi zima la Ufundi la Yanga. Hawana 'Plan' B ya kuifungua Timu inayozuia kwenye 'Low Block'
9: Bado Mchezaji muhimu kwenye kikosi cha Yanga msimu huu atabaki kuwa YANICK BANGALA. Jinsi alivyokuwa anaitoa timu na kuiunga kwa viungo wake ni sanaa ya viwango vya juu sana 🙌
10: Well Done Mwihambi👏 Well Done Asukile na Mwashilindi. Jasho lao limevuja haswa! Ile ndio DNA ya Prison wanapokuwa kwenye wakati mgumu kiwanjani
Nb: Wameacha Kutetema.. wameanza KUTETEMEKA 😃
Post a Comment