1: WHAT A MATCH..CLASSIC🙌 Baada ya stori za Ambulance, vifungo vya makocha unahitaji Dakika 90 za aina kuthibitisha UBORA WA LIGI YETU UWANJANI
2: Asante Moalin. Asante Pablo Franco👏 Mechi ilichezwa sana kwenye mbinu kisha ikamalizikia kwenye Ufundi wa wachezaji. Kila shabiki wa soka AMEENJOY BOLI✊
3: Azam walikuja na sapraiz ya 3-5-2 huku Simba wakija na mfumo wa 4-3-3. Kwanini kipindi cha kwanza walionekana kuikamata mechi?
4: Dube na Kola walikuwa superb sana kwenye System hii. Runs za Dube aliyekuwa anashuka chini kidogo kufata mpira kuliifanya Azam walioverload eneo la lati .. Ikawa Battle ya 4v3 na sio 3v3 kama Pablo alivyofikiria iwe. Movements za Kola zikawa zinamtoa sana Onyango na Henock kwenye shape yao ya ulinzi
5: 'Second Half' Levo ya kasi ya mchezo ilipanda sana. Pablo akayatumia mapana ya uwanja kwa kumchagua Banda kukimbia nyuma ya Lusajo! Ni kipindi ambacho makocha wote walihitaji Quality ya mastraika wao kushinda mechi lakini hawakuipata
6: KENNETH MUGUNA.. WHAT A PLAYER🙌 WHAT A PERFOMANCE👏 Alikontroo mechi kwenye ubongo wake. Alikimbia kulia na kushoto kusambaza upendo katikati ya uwanja. Usahihi wa pazi zake kwa asilimua kubwa ndio ulikuwa usahihi wa plan ya Azam kwenye kushambulia
7: Prince Dube.. Alichokosa ni bao tu.. Lakini Perfomance yake ni TOP KABISA. Movements zake, Ukokotaji wake wa mpira na uwezo wake wa kushinda 1v1 uliwapa wakati mgumu sana mabeki wa Simba.. Ni kocha wa Azam pekee anayejua kwanini Dube hakustahili mechi..!
8: Napenda kazi ya Muzamir Yassin kipindi hiki.. Kanoute alirudi vyema lakini ni kama hakuwa fiti 100%.. Kwa mara nyingine tena Bwalya anashindwa kuwa msaada wa Simba pindi anapohitajika kufanya hivyo
9: Dennis Kibu alishika mpira. Ilistahili kuwa Penalti. Pengine mwamuzi Herry Sasi hakuwa kwenye 'Position' nzuri ya kuliona tukio.. Lakini Azam walistahili kupata ile penalti
10: Mechi nzuri Sospeter Bajana.. 👏 Mechi nzuri Aishi Manula.. Nilipenda sana Show za Kapombe na Kangwa
Nb: Kumbe Wanateseka sana Bila kuwasha moto 😃
Post a Comment