Abiria Aendesha Ndege, Rubani Alipoteza Fahamu



Siku ya jumanne wiki hii, abiria aliyekuwa ndani ya ndege bila mafunzo yoyote ya urubani, alifanikiwa kuendesha ndege kutoka Bahamas mpaka katika mji wa Florida nchini Marekani baada ya rubani wa ndege hiyo kupoteza fahamu.
Ndege hiyo ndogo ya injini moja ilikuwa na rubani mmoja na abiria wawili. Baada ya rubani kupoteza fahamu abiria mmoja alienda katika sehemu ya rubani na kupiga simu kuomba msaada.

Simu yake ilipokelewa na waongoza ndege wa uwanja wa ndege wa Palm Beach katika mji wa Florida na kumpa maelekezo mpaka akafanikiwa kufika katika uwanja huo na kutua salama bila tatizo lolote kutokea.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post