Zari Hassan na Wema Sepetu Faida Kwa Mondi



Zarina Hassan 'Zari' na Wema Sepetu 'Maadam'. Wote 'wameshea' mbavu za Abdul Naseeb 'Diamond Platinumz'. Licha ya mshikaji kupita na pisi kibao zenye viwango. Lakini hawa wameacha alama zao kwake.

ZARI
Alijitenga na mbavu za Mondi miaka michache nyuma. Akizidiwa na fujo za dogo ambaye ana kila kitu kimaishani. Maisha ambayo kila kijana anayatamani au kuyaota. Yes yuko vizuri na Misa siyo kitu cha ajabu kwetu alipovamia anga la mwenzake miaka kadhaa nyuma. Mawe.

WEMA
Penzi lake kwa Mondi liliingiliwa sana na pisi kadhaa za mjini, hasa mastaa wenzake. Lakini alitoka na kurudi kwa Mondi mara kadhaa na kukomaa. Ujio rasmi wa Zari pale Madale, ulifanya Wema akae mbali na mbavu za Mondi jumla jumla. Kifupi hajawahi tena kuwa na thamani ile mbele ya uso wa Mondi.

ZARI
Kampa heshima Mondi kwa kumzalia watoto wawili. Na kuwatuliza wanoko waliosema mwana mgumba. Kabla ya Zari, alitoka na pisi kibao bila matokeo. Zari kampa heshima na maujanja ya kujiongeza zaidi kimaisha. Lile ting'a la "Zari All White Party" pale Mlimani City unalikumbuka?

WEMA
Alimpa penzi na umaarufu.uliofanya hata Zari akamjua. Akampa kiingereza cha kuwasiliana kimataifa. Yes! Wema anajua sana lugha na alikuwa staa zaidi ya Mondi kabla. Na kiki kibao za Wema zilitengenezea pesa zaidi kwa Mondi. Vuta kumbukumbu ya show kubwa ya kwanza ya Mondi, "Diamond Are Forever" pale Mlimani City. Amazing.

MONDI
Shughuli zake, umaarufu wake, pesa zake, umri wale na njaa za wadada wa mjini. Ni vigumu sana kutulia. Labda iwe pisi yenye upungufu wa akili, ndo itaweza kuhimili presha za msela huyu. Lakini hata Wema na Zari, wote wako nje ya uwanja wa Mondi kihisia.

"Haya ndo mapenzi yenye faida na maisha kwa mwanaume."



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post