Vikwazo mimeendelea kuwekwa katikan shughuli za Will Smith kufuatia tukio la kumchapa kofi mchekeshaji Chris Rock wakati wa utolewaji wa tuzo za Oscar 2022 huko nchini Marekani.
Licha ya kuomba radhi hadharani na kwa kutumia mitandao yake ya kijamii na hata muathiriwa Rock, kutoonesha haja ya kushitaki juu ya tukio hilo mambo yanaonekana kumgeuka Will Smith
Taarifa mpya kumuhusu muigizaji huyo zinasema kuwa mpaka sasa kampuni maarufu ya uzalishaji na usambazaji wa filamu kwa njia ya mtandao ‘Netflix’ imesimamisha mkakati wa utengenezaji wa filamu mpya ya Will Smith ‘Fast and Loose’.
Kwa upande mwingine suala hilo ni kama muendelezo wa kukwama kwa filamu hiyo ambapo kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika inaelezwa kuwa filamu hiyo ilianza kupoteza nuru ya kukamilika kwake kufuatia kuondoka kwa aliyekuwa muongozaji, hivyo wakati kampuni hiyo ikimtafuta mtu wa kuichukua nafasi ya muongozaji ili kuendelea na mradi huo ndipo suala la ‘kofi’.
Sakata la muigizaji Will Smith kumchapa kofi mchekeshaji Chris Rick akiwa jukwaani wakati wa ugawaji wa tuzo za Oscar za 94, lilisababishwa na utani aliutoa Rock akiuelekeza kwa mke wa Smith Jadda Pinket kitendo ambacho hakikumfurahisha Will kiasi cha kuamua kupamda jukwaani na kumshushia kichapo cha kofi moja usoni.
Post a Comment