Wema: Siwezi Kuishi Watakavyo Wao “Mimi Sijaona Tatizo Kwenye ile Video na Davito”



Mwanadada Wema Isaac Sepetu.
Baada ya video yake kusambaa akiwa na mwanaume anayejulikana kwa jina la moja la Davito, hatimaye mwanadada Wema Isaac Sepetu amesema watu waache kufuatilia maisha yake.

Akizungumza na Gazeti la IJUMAA, mrembo huyo mwenye mvuto wa aina yake, anasema kuwa, anashangaa watu wanavyomjadili utafikiri wameona kitu gani cha ajabu, wakati yule ni rafiki yake tu kama walivyo rafiki zake wengine.

“Mimi sijaona tatizo kwenye ile video, tulikuwa sehemu tuna-enjoy na Davito ni mshikaji wangu, sasa sijui cha ajabu nini hapo, sitaki kufuatiliwa maisha yangu, naomba waniache kwa sababu siku zote siwezi kuishi vile ambavyo wao wanataka,” anasema Madam Wema.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post