Wema Aibua Sababu Mastaa Kutoolewa, “Mastaa Waponzwa na Tabia zao za Kuiga”





Wema Isaac Sepetu wengine wakimuita Tanzania Sweetheart au Last Born wa Taifa.
Kuwa na mwenza maishani ni jambo zuri kwa kila mwanamke au mwanaume.

Kupata mtu wa kukuoa au kuoa ni baraka. Inakuwa ngumu wakati watu wanazeeka, lakini hakuna wa kumpenda au kumpa hisia zake kama mwanamke au mwanaume.

MASKINI WEMA

Ndivyo ilivyo kwa Wema Isaac Sepetu wengine wakimuita Tanzania Sweetheart au Last Born wa Taifa ambaye ni supastaa grade A wa Bongo Movies.

Maskini Wema; bidada amewashangaza mashabiki wake baada ya kutoa kilio chake cha kukosa mwanaume wa kumuoa akidaiwa kutonesha vidonda vya mastaa wengi kwenye ulimwengu wa mastaa Bongo ambao hawajaolewa.


 
Wema anasema kuwa anatamani kuolewa, lakini tatizo pekee ni kwamba hakuna mwanaume wa kumuoa.

WEMA: TATIZO BWANA HARUSI

“Jamani natamani kuolewa…Yaani nimetamani tu harusi….Na iwe exquisite…the thought of me in a wedding dress, watu wamependeza…food and drinks na good music…Daaaaah…

“Bibi Harusi nipo, tatizo ni bwana harusi….Bado hajajitokeza….,” anasema Wema kwa uchungu wakati huu akielekea kutimiza umri wa miaka 33; kwani amezaliwa Septemba 28, 1990.

Wema kwa sasa yupo singo kwa sababu hajamtambulisha mtu wake rasmi tangu alipotengana na staa wa muziki nchini Tanzania, Diamond Platnumz.

Kuachana kwao kulikuwa pigo kubwa baada ya hapo hawakuzungumza kwa miaka mitatu, lakini sasa ni wapenzi zilipendwa wanaopendwa zaidi ambapo mwaka huu walitwaa Tuzo ya Ma-x Wanaopendwa 2022.

KIAPO CHA DAMU NA DIAMOND

Wema na Diamond walidumu yapata miaka miwili tangu 2012 hadi 2014 ambapo walikula hadi kiapo cha damu ili wadumu milele, lakini mambo hayakwenda sawia.

WEMA NA SABABU MASTAA KUTOOLEWA

Kilio cha Wema kinakuja wakati huu kukiwa na wimbo kubwa la mastaa wa kike Bongo ambao nao wanalia kutoolewa


 
Kwa mujibu wa uchunguzi wa IJUMAA WIKIENDA, zipo sababu mbalimbali zinazowaponza mastaa walio wengi zinazosababisha kukosa wa kuwaoa.

Kwanza, baadhi ya mastaa hao inasemekana wanaponzwa na tabia zao za kuiga zinazoaminika haziendani na matakwa ya jamii kuanzia uvaaji, ukaaji, viwanja vya starehe, lugha zisizo nzuri, marafiki na mengine ambavyo husababisha kuhatarisha nafasi yao ya kupata mume.

Imebainika kwamba, wanaume wengi huwa hawapendezwi na tabia za aina hiyo hata mwanamke awe mrembo kiasi gani kama walivyo baadhi ya mastaa hao.

Baadhi ya mastaa hao wanasemekana kuwa na dharau mno kwa wanaume wanaowafuata wakitaka kuwaoa.

Wengine inasemekana siyo wife material (mke bora); wapo ambao hawawezi hata kuosha vyombo, kufanya usafi wa nyumba au kufua kwa kuogopa kucha zao zisikatike.

Wengine hawajui kupika kwa kuogopa kucha zao zisikatike.

Wengine hawajui kupika na hawawezi kulea watoto kwa kuogopa kuchafuka.

Inasemekana baadhi yao ni ghali kuwatunza kwa sababu huwa na dhana kuwa wanafaa kupelekwa katika hoteli kubwakubwa na maeneo yaliyo na bidhaa ghali.

Huwa hawalegezi msimamo hasa kuhusu mahitaji yao na wanakotaka kwenda kununua bidhaa.


 
Wengine inasemekana kinachowaponza ni kufikiri dunia ni yao na kwamba wanafaa kuabudiwa na kila mwanaume.

Wanaume wengi hawapendi wanawake wa aina hiyo ambao huwadharau kutokana na kuwa wanapendwa na wanaume wengi.

GPL


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post