Tangazo la EP ya Diamond Platnumz FOA Kwenye Basi Uingereza


Supastaa @diamondplatnumz anaendelea kutunisha misuli Kimataifa. Mara hii ni kuhusiana na tangazo la EP yake "First Of All" ama #FOA kuwa kwenye usafiri wa umma huko Uingereza.

Hilo limewekwa wazi na meneja wa mkali huyo Sallam SK ambaye kwasasa yupo na Diamond huko London, Uingereza kwaajili ya shughuli zao za kimuziki.

@sallam_sk ame-share kupitia insta story yake Basi hilo lenye tangazo la EP ya Diamond likiwa kwenye mitaa ya huko London, Uingereza.

Diamond ambaye aliwahi kusema hapendezwi kushindanishwa na wasanii nchini kutokana na kuwazidi katika maeneo makuu matatu; ambayo ni mauzo, shoo za kimataifa na maendeleo (mali) yatokanayo na muziki, hii ni hatua nyingine anayoionyesha kuwa anaimba na kutafuta wateja wakumsikiliza popote duniani.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post