Paula Afunguka Mapya Atoa Kijembe “Labda Nife Ndo Mama Amrudie Harmonize”




Kajala akiwa na mama yake Kajala.
Paula Kajala; ni mrembo maarufu kwenye mitandao ya kijamii (sosholaiti) na ni binti wa mwigizaji wa Bongo Movies, Kajala Masanja ambaye naye ameingilia kati sakata la mama yake huyo kusemekana amemrudia Harmonize.

Paula au Pau anadaiwa kuwa kikwanzo kikuu cha Kajala kurudiana na Harmonize kwa sababu yeye yupo na msanii Rayvanny ambaye ni hasimu mkubwa wa Konde Boy.

Kwa mara ya kwanza, kupitia Insta Story, Paula amesema; “Over my died body (bora nife), tuko zetu uchagani…” Kisha akamtagi mama yake, Kajala.

Sasa hapo ndipo wajuzi wa mambo wanasema hicho ni kijembe kwa Harmonize kwamba mama yake hawezi kurudi.


 
Hata hivyo, baadhi ya watu wamemshambulia Paula kwa kumtaka kukaa mbali na mambo ya watu wazima hivyo aache kabisa kuingilia mambo ya mama yake ya kimapenzi.

Stori; Khadija Bakari, Dar



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post