Nini Kikwazo Cha Harmonize Kufikia Malengo yake ya Kuwa Msanii Namba Moja?


Harmonize amekuwa akitamani kutawala soko la mziki Tanzania , amejitahdi Sana Kwa Kiasi chake ,media kubwa zinampigia promo, pia baadhi ya account maarufu za wambea wa Instagram zipo nyuma yake.

🍁Kuna watangazaji pia ambao licha ya kuonekana kama wehu mfano mwijaku (Msomi😂) lakin hawajali na ni kama wamejitoa kafara kumsupport kijana.

🍁Pamoja na hayo yote nguvu aliyowekeza konde inaonekana kuleta matokeo madogo, hapa najaribu kulinganisha ukubwa wa uwekezaji aliyoufanya na output inayotoka zaidi ya miaka miwili sasa, huu ni muda mzuri kabisa kwa matazamio.

🍁Kwa miaka miwili Harmonize Hana tuzo yoyote kubwa na ya maana na sioni record ya Harmonize popote pale kwenye mziki hapa Africa ,

🍁Harmonize amesha mtuhumu Diamond kama mtu anaemfanyia fitina za chini chini lakini kumbuka Diamond ndio mtu pekee aliyeiona thamani ya Harmonize mda ambao wadau wote wa Mziki walimuona hawezi.

🍁YouTube imekuwa ndio kipimo cha kukubalika Kwa msanii, msanii anapokuwa na numbers nyingi inaaminika kuwa amekubalika sana na wadau. Ila kwa harmonize mapokeo ni madogo kulingana na kujinadi kwake kuwa ndio number one artist

Unahisi Harmonize ni nyota hana au ni wadau wa mziki wanampotezea?



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post