Mwanamuziki Ibraah wa Konde Music Worldwide ameweka bayana kuwa angependezwa sana na kufufuka kwa mahusiano kati ya bosi wake Harmonize na mwigizaji Fridah Kajala Masanja.
Ibraah ambaye kwa jina halisi ni Ibrahim Abdallah Nampunga amekiri kuwa moyo wake unaumia kuona jinsi mdosi wake anavyohangaika.
"Kwa kweli natamani Kajala arudi nyumbani kwa sababu ni furaha ya ndugu," Ibraah alisema akiwa kwenye mahojiano na Carrymastory.
Ibraah aliweka wazi kuwa kwa kawaidai huwa hahusiki na masuala ya kifamilia ya Harmonize na hana ufahamu mzuri wa yaliyotokea kati yake na Kajala. Hata hivyo alimwomba mwigizaji huyo msamaha kwa niaba ya bosi wake na kumsihi amrudie.
"Kama binadamu, kwa kweli najisikia vibaya kwa sababu ndugu anajisikia vibaya. Kama ingewezekana kumwomba msamaha basi namimi nimwombe msamaha Kajala. Msamehe kakangu kama alikukosea," Alisema.
Mwanamuziki huyo alipuuzilia mbali madai kuwa Harmonize ametia bidii kubwa zaidi katika kurejesha mahusiano yake na Kajala na kusahau kazi ya kusaidia wasanii wake wa Kondegang.
Alimshauri bosi huyo wake kuheshimu hisia zake na kuwa makini na jinsi anavyoshughulikia mambo yanayomkabili.
"Kila mtu ana matakwa yake. Kama anampenda kwa kweli anahitaji kupambana kwa kuwa anampenda," Alisem Ibraah.
Ibraah aliweka wazi kuwa licha ya yanayoendelea, hana wasiwasi wowote kuhusiana na Harmonize kushindwa kuendeleza kazi zake.
Katika kipindi cha takriban mwezi mmoja ambacho kimepita Harmonize amekuwa akifanya juhudi kubwa kumwomba msamaha Kajala na kumsihi warudiane.
Tayari ameweza kuweka bango lao barabarani, kumnunulia mkufu ghali, gari aina ya Range Rover kati ya mambo mengine makubwa.
Post a Comment