Nabi Aikunia Kichwa Namungo Nakusema Haya


i
KOCHA Mkuu wa Yanga, Nesreddine Nabi amewaangalia wapinzani wao, Namungo FC na kusema wanahitaji kujiweka fiti zaidi kuhakikisha wanafanikiwa kupata pointi tatu katika mchezo dhidi yao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Akizungumza na gazeti hili jana, Nabi alisema hakuna mechi iliyokuwa rahisi mbele yao hasa wanapokwenda kukutana na timu ambayo iliwasumbua katika mzunguko wa kwanza.

Alisema katika mechi ya kwanza walitoka sare ya 1-1 wakiwa ugenini, ana imani watakuwa wamebadilika kwa sababu wamefanya mabadiliko benchi la ufundi na kuwa na kiwango bora zaidi.

“Namungo FC ina wachezaji wazuri ukiangalia benchi la ufundi tofauti na mechi ya kwanza, tunatakiwa kujiandaa kuhakikisha tunafikia malengo yetu ya kupata pointi muhimu katika michezo iliyopo mbele yetu,” alisema Nabi na aliongeza.

“Kazi kubwa kwa sasa kuendelea ni kujiimarisha zaidi kila nafasi ukiangalia katika mechi iliyopita kuna baadhi ya wachezaji akiwemo Saido Ntibanzokiza na Fiston Mayele kucheza wakiwa wagonjwa,” alisema Nabi.


Alisema baada ya mapumziko ya siku chache timu imerejea kambini ameona nyota hao na baadhi ya majeruhi kurejea uwanjani na matumaini makubwa ya mechi ijayo kuwa na kikosi kipana.

Nabi alisema kazi kubwa anayoifanya kwa sasa anaendelea kuisuka safu ya ushambuliaji kuwa imara na kurejea ilivyo awali kushinda kila mechi katika ligi hiyo.

Yanga inashuka dimbani Aprili 23, mwaka huu ikiwakaribisha Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu mzunguko wa Pili utakaopigwa, Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post