Mwigizaji wa Nigeria Chioma Toplis Amtapikia Nyongo Baba yake Mzazi Kwa Kuwa Katili kwa Mama yao Ndani ya ndoa


Mapya yaibuka 😲😲! Mwigizaji wa Nigeria Chioma Toplis amtapika baba yake mzazi mwanzo mwisho kwa kuwa katili kwa mama yao ndani ya ndoa

Kifo cha mwimbaji injili maarufu Osinachi Nwachukwu kimeendelea kuibua mambo mengi na kuwa mjadala maarufu barani Africa kuhusu unyanyasaji wa majumbani(domestic violence)

Juzi kijana mmoja wa kiume Nigeria aliibuka kumlaani baba yake mzazi ambaye ni mzee wa kanisa kwa kumnyanyasa mama yake hadi akafariki dunia huku kijana huyo akisema viongozi wa dini wa kanisa alilokuwa akisali mama yake walikuwa wakimhimiza mama yake avumilie ndoa hadi mauti yakamkuta kwa kupigwa na baba yake na baada ya muda baba yake akaoa mwanamke mwingine

Dada mwingine wa Nigeria na yeye ameibukia Twitter kusema kwamba na yeye baba yake mzazi alikuwa mzee wa kanisa na alifariki miaka 9 iliyopita ila hakumlilia na hatokuja kumlilia sababu alishuhudia jinsi alivyokuwa akimnyanyasa mama yake mzazi hadi mama yake akaikimbia ndoa kunusuru maisha yake na anaendelea vizuri na maisha yake

Sasa hapa ndipo Mwigizaji wa Nigeria Chioma Toplis na yeye alipotema nyongo kuhusu baba yake mzazi.

Chioma anasema hata yeye baba yake ni mzee wa kanisa lakini amekubuhu kwa unyanyasaji nyumbani, amesema ameshaapa hatokuja kumzika baba yake mzazi kwani baba yake huyo amejaa ujinga, uvivu, kupiga wanawake, umalaya, kutokujielewa na hana chochote cha maendeleo cha kujivunia katika maisha

Chioma ameendelea kusema kwamba hata siku baba yake akifariki hakuna kitakachofanyika kwenye mazishi yake zaidi ya kumuingiza tu shimoni afukiwe. Amesema siyo yeye tu bali hata ndugu zake wengine wanamchukia sana baba yao na hawatafika kwenye mazishi yake sababu wameona jinsi alivyomnyanyasa sana mama yao, isipokuwa ndugu yao wa kiume tu ambaye ndie mtoto wa kiume wa Kwanza ndie atakayehudhuria mazishi ili kukamilisha taratibu za kimila na si Kingine. Anasema na wanaini baba yao ndie atatangulia kufariki

Amesema hilo si geni na anaongea akiwa na akili zake timamu na hata huyo baba yao mzazi anajua hilo kuwa hawatahudhuria masishi yake sababu ya ukatili alikuwa aliokuwa akimfanyia mama yao



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post