Msanii Wizkid Akunja Zaidi ya Shilingi Bilioni 2 Kuwa Msanii Kinara Tamasha la Rolling Loud


Mwimbaji wa Nigeria Wizkid ametajwa kwenye orodha ya wasanii watatu vinara (headliners) ambao watatumbuiza kwenye tamasha la Rolling Loud ambalo litafanyika September 9-11 mwaka huu mjini Toronto Canada.


Mbali na Wizkid kuna Future na Dave ambao ndio wanakamilisha idadi ya headliners watatu wa tamasha hilo lenye mamia ya wasanii wakali toka nchini Marekani ambao watapanda Jukwaani.


Kubwa hapa ni kiasi cha pesa ambacho Wizkid amelipwa kutumbuiza kama msanii kinara, kupitia insta story yake amesema amelipwa ($1 million) zaidi ya Shilingi Bilioni 2.3 za Kitanzania.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post