Akiambatanisha picha ya tuzo hiyo ambayo ni ya silver, kwenye post yake Instagram ameandika, "Asanteni sana mashabiki wangu, asanteni youtube kwa zawadi. Ni hatua nzuri katika safari yangu ya muziki. Naomba muendelee ku-subcribe Asante."
Amber Lulu ambaye ni mzaliwa wa jijini Mbeya, alijiunga na mtandao Youtube Disemba 27, 2016 na amepata wafuasi (subscribers) wengi kutokana na kazi zake mbalimbali anazoziweka katika mtandao huo.
Amberlulu katika channel yake ya Youtube ana jumla ya video 35, zenye jumla ya views Milioni 9,713,861. Anaingia kwenye top 10 ya wanamuziki wakike Tanzania wenye wafuasi wengi katika mtandao wa youtube wakiongozwa na @officialzuchu mwenye wafuasi (subscribers) milioni 1.94
Post a Comment