Majizo Atoa Neno Kwa Harmonize "Umekuwa Mdogo Wangu.. Kuomba Msamaha na Kurekebisha Ulipokosea Huo ni Ukomavu"



Mkuregenzi wa vituo vya habari, Efm pamoja na Tv E, @majizzo ametumia ukurasa wake wa Instagram kuongelea kitendo cha msanii @harmonize_tz
Cha kuzidi kumuomba msamaha aliyekuwa mpenzi wake, @kajalafrida huku akikitazama kitendo hicho kwenye mtazamo wa uungwana zaidi kuliko wengi wanavyo kitazama kama Kiki, Mswahili ameandika👇

“Okay suala la Konde, kwangu lina sura ya utu zaidi kuliko sura ya muziki (game) kama wengine wanavyoliona.

Nje ya muziki na biashara, umaarufu na kila kitu, huyu NI MTU. Ni Rajabu, ana wazazi, ana moyo wa kupenda.

Hii video imenigusa sana. Kanyoosha maelezo niliyokuwa nayakosa kutoka kwake na nadhani anafufundisha kitu:

1. Binadamu mwenye uungwana, akitambua kosa lake anaomba msamaha. Harmonize alikosea na makosa yake yalienda public. Alitakiwa kuomba msamaha, na ikibidi hadharani. Kafanya hivyo : Kwa nini atukanwe?

2. Anaonesha kwamba anampenda Kajala kwa dhati, Je tutamhukumu kwa sababu ya kupenda?. Kila mtu ana namna yake ya kuelezea mapenzi yake, kwa kuwa hakosei mtu hastahili kejeli.
.
Hapa palipofikia, anayeweza kumsaidia Harmonize amsaidie. Tusisubiri mabaya yamfike. Mimi nitajaribu kwa namna yangu, na Kajala akitusikia na kuamua kusamehe nitashiriki kikamilifu ndoa yao.
.
@harmonize_tz umekua mdogo wangu, hongera ukomavu wa kuomba msamaha na kutaka kurekebisha ulipokosea. Pambania penzi lako.”


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post