Mashabiki wamemcharukia vibaya mwanasosholaiti na mfanyibiashara, Zari baada ya kupakia picha katika mtandao wa Instagram akionyesha mazingira ya kijijini kwao huko Uganda.
Kulingana na picha hizo, baadhi ya mashabiki walikisia kwamba Zari amewatelekeza wazazi wake licha ya kuwa na ufanisi mkubwa kimaisha.
"Jengeni na kwenu kuna Leo na kesho😂," shabiki mmoja aliandika
Asilimia kubwa ya mashabiki walisema kwamba, staa huyo anaishi maishi ya raha huku wazazi wake wakipitia taabu na kuishi maisha duni huko kijijini.
Wengine pia hawakusita kuachia cheche zao wakidai kwamba Zari amesota ndo maana ameamua kurudi kijijii.
Kwa upande wake Zari, alionekana kutofurahishwa a kauli hizo na kumzomea vibaya shabiki mmoja aliyetuma ujumbe kwenye ukurasa wake.
"...Nimekuekea picha za nyumba ya wazazi wangu huko Sapchat, enda ukaangalie halafu ukome kabisa kutia pua yako kwa mambo ya watu yasiyokuhusu," Zari aliandika.
Baadhi ya mashabiki pia waliandika jumbe za kumpongeza Zari kwa bidii anazotia katika mishe zake, na kwamba hajasahau alipotoka licha ya umaarufu wake.
"...Wewe ndiye mwanamke mzuri zaidi nishawahi kukutana naye maishani, licha ya mali uliyo nayo bado unakumbuka ulikotoka," shabiki alimwambia.
Post a Comment