Huku akiwa kwenye mahojiano Harmonize alidai kwamba anamheshimu Diamond sana na kwamba ana mshukuru kwa kukuza taakuma yake ya mziki.
"Licha ya kuwa kaka na rafiki yangu, kama katika uhusiano mwingine wowote hatuko karibu tena na ni jambo la kawaida. Sina lolote dhidi yake. Namheshimu sana Diamond kwa kunitia moyo na kunishauri kimuziki. Nina deni kwake kwa kuwa chanzo cha mafanikio ya muziki wangu,” alisema Harmonize.
Aliongeza zaidi kuwa;
"Nilipokuwa chini wakati wa hatua za awali za kazi yangu ya muziki, tulikuwa hatutengani. Diamond alijitahidi sana kuunga mkono na kukuza kazi yangu ya muziki. Nina deni la mafanikio yangu kwa Mungu na Diamond,” anasema na kuongeza kuwa kama ishara ya kumshukuru ana tattoo ya Diamond kwenye mkono wake."
Post a Comment