Msanii na mtangazaji kutoka Tz, Babalevo amesema kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa Harmonize kurejeleana na mpenzi wake wa zamani, Frida Kajala.
Alisema kwamba licha ya mambo mabaya aliyoyapitia Kajala kipindi yupo kwenye mahusiano na Konde, kuna ishara tosha kwamba atamsamehe na kukubali kufufua penzi lao.
"...Unazungumzia Kajala sio? Ninavyoona atakubali kurudiana na Harmonize," Babalevo alisema.
Babalevo alisema kwamba ni rahisi kwa mwanamke kusamehe mwanaume anapofanya kosa, kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa Kajala akakubali kuyeyusha moyo na kuliendeleza penzi lao.
Ikumbukwe Harmonize alikiri kwamba ameshindwa kufunga katika kipindi hiki cha Ramadhan kwa sababu ana mawazo mengi kuhusu Kajala na angependa sana kumnasa tena katika himaya yake ya huba.
Licha ya vurugu zilizotokea wakati wanatengana, ni wazi kwamba penzi kati yao lilikuwa limekolea sana.
Mpaka sasa Kajala hajatoa tamko lolote iwapo angependa kurejeleana na 'tembo' , huku mashabiki wakisubiri kwa hamu kuona hatua atakayoichukua.
Post a Comment