Kupitia Ayo Tv, Muongozaji wa music Video nchini, Director Kenny amefunguka baadhi ya sababu zilizo fanya aache kufanya kazi na Diamond,huku akiweka bayana ni nani mtu wa kwanza kuja na wazo la Zoom Production.
Kenny amedai mtu wa kwanza kabisa kuja na wazo la Kuanzisha Zoom Production alikuwa ni msanii Harmonize na baadae akamkutanisha na Diamond Platnumz kwakuwa Harmonize alikuwa kwenye label ilikuwa ni lazima uongozi ujue, Diamond akavutiwa na project na kuwa partner, Kipindi hicho Harmonize amemtoa Kenny kwa Hanscana.
Kenny Amedai si kuwa alimsaliti Harmonize baada ya kuondoka WCB, bali mwisho wa siku kinacho tafutwa ni maisha, kulikuwa na opportunities nyingi kufanya kazi na Diamond kwa wakati ule kuliko Harmonize.
Kingine Kenny amedai kitu kilicho fanya aache kufanya kazi na Diamond na kwenda kuanzisha kampuni yake, ukiacha sababu nyingine, Tatizo kubwa lilianzia wakati wanashoot video ya Gimmie aliyofanya na Rema . kwa siku tatu watu hawakulipwa pesa zao, na kila mtu ana sehemu yake na alipaswa kulipwa, Diamond alipokuwa akiambiwa hakuonyesha ushirikiano mzuri, ishu hii ilifanya kila mtu kukasirika na ukizingatia gharama ya video zake ni kubwa.
Kenny hajafafanua kama kutumika mzazi mwenzie kama video vixen kwenye video ya Diamond bila ridhaa yake,ni miongoni mwa sababu zilizomtoa WCB
Post a Comment