Chelsea, Bayern Munich waiaga kwaheri Champions League




Mabingwa mara sita wa Champions League Bayern Munich na mabingwa mara mbili Chelsea walipungia kombe hilo mkono wa kwaheri usiku wa Jumanne katika mkondo wa  robo fainali.

Safari ya Bayern Munich ilifika ukingoni  baada ya kushindwa kupata ushindi nyumbani dhidi ya Villareal.

Mechi hiyo ambayo ilichezwa mwendo wa saa nne usiku iliisha kwa sare ya 1-1 hivyo kufanya jumla ya mabao kuwa Bayern 1, Villareal 2. Vijana wa Unai Emery walipata ushindi wa 1-0 katika mechi ya mkondo wa kwanza.


Real Madrid iliponea chupuchupu kubanduliwa nje ya kombe hilo baada ya mshambulizi Rodrygo kufunga bao muhimu katika dakika ya 80.

Bao la Rodrygo lilifanya mchuano huo uende hadi dakika za maongezi ambapo Benzema alifungia Madrid bao la pili na kuipa klabu hiyo ya Uhispani ushindi wa 5-4 kwa jumla.

Villareal na Real Madrid wanasubiri kujua washindani wao katika nusu fainali ambao watapatikana kutoka kwa mechi mbili zitakazochezwa usiku wa Jumatano.

Atletico Madrid watakaribisha Manchester City ugani Wanda Metrapolitano mwendo wa saa nne huku Benfica wakiwa wenyeji wa Liverpool ugani Anfield.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post