Baada ya Serikali kurejesha Tsh. 100 ya tozo katika mafuta, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei mpya ya Petroli kwa Dar es Salaam itakuwa Tsh. 2,861 kutoka Tsh. 2,540 ikiwa ni ongezeko la Tsh. 321
Mkurugenzi wa Petroli wa EWURA, Gerald Maganga amesema upande wa Dizeli bei mpya itakuwa Tsh. 2,692 kutoka Ts.h 2,403 ongezeko likiwa ni Tsh. 289, Mafuta ya Taa Tsh. 2,682 kutoka Tsh. 2,208 ongezeko ni Tsh. 474
Maganga ameongeza kuwa mafuta ambayo yatapitia Bandari ya Tanga, bei ya Petroli itakuwa Tsh. 2,848, Dizeli Tsh. 2,779 kwa lita moja huku Mafuta ambayo yatapokewa kupitia Bandari ya Mtwara, Petroli Tsh. 2,678 na Dizeli Tsh. 2,811
#JamiiForums
Post a Comment