Alikamwe "Mambo 10 nilioyaona Polisi vs Simba, Gape ni Point ni 10"


Mambo 10 nilioyaona Polisi vs Simba

1: 'GAPE ni POINTI NI 10' Pale kileleni. Kimahesabu bado Ubingwa uko wazi, Lakini kwenye Uhalisia.. Hii suluhu na Polisi inaweza kuwa imeamua Bingwa wa Msimu huu.. Huu ndio ukweli ambao shabiki wa Simba hawezi kuusema kwa sauti.

2: Simba ni kama akili/nguvu iko CAF. Interview ya kocha Pablo kwa kiasi fulani imethibitisho hilo. Kikosi kilichoanza kilipangwa kimkakati wa kuisubiri ORLANDO na sio kuikimbiza YANGA..

3: Mbaya zaidi hata wachezaji walionekana kuiwaza CAF. Baadhi walicheza kwa Tahadhari ya kukwepa majeraha. Polisi wakawa na Faida ya kushinda kwa asilimia kubwa mipira ya 50-50

4: Ile 'PITCH' YA USHIRIKA sio Rafiki. Nimemsikia mpaka Kocha msaidizi wa Polisi amesema mpira umeshindwa kuchezwa vyema kwa sababu ya eneo la kuchezea. Good Football huwezi kuipata pale..

5: Tactically Simba walitoka kwenye mfumo wao wa 4-2-3-1 na kuja na 4-1-3-2 kwa ajili ya kupambana na mazingira ya Uwanja. Kibaya kwao ni kama wachezaji hawakupata muda wa kutosha kwenye uwanja wa mazoezi kuuelewa mfumo huu. Kiasi walipata shida kuutekeleza.. Japo 'Rotation' kubwa ya kikosi ni Factor nyingine inayoweza kuwekwa mezani

6: POLISI walirudi kwenye 4-2-4 .. Mfumo wao pendwa! Vitalis Mayanga akicheza kama Namba 10, Tariq Simba na Deus Cosmos wakicheza kama viungo wawili wa kati. Mfumo huu una faida kwa Polisi kwa sababu ya wachezaji wao wawili wa pembeni

7: Kasi KASSIM HARUNA na SALIBOKO kwenye mapana ya Uwanja inawapa urahisi viungo kutupa mipira pembeni. Kasi yao, nguvu ilikuwa kizingiti kikubwa kwa mabeki wa pembeni wa Simba

8: Polisi ni kama wameipoteza nafasi ya dhahabu ya kupata ushindi mbele ya Simba. Walipoteza nafasi nyingi za wazi za kuiamua mech.. Labda walicheza kwa presha kubwa, umakini ukapungua.

9: Mabeki wa pembeni wa Polisi.. Yahya Mbegu, Datius Peter.. Mechi nzuri sana kwao.. Hongera pia kwa Beno Kakolanya.. Alikuwa na 'Timing' nzuri sana kwenye kusoma shambulizi la Polisi

10: Kennedy Juma anaonyesha kuwa anahitaji dakika zaidi. Gadiel anaonyesha pia anatakiwa kuimprove zaidi..

Nb: Kuna Tofauti ya msemaji aliyezoea kubeba Ubingwa na aliyezoea Kubeba Simu ..😃


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post