1: WHAAT A MATCH! WOW .. JUST WOW! Ile ndio Standard Tunayoitaka kwenye Ligi yetu🙌 BRAAAVO kwa Makocha na Wachezaji wa Timu zote mbili. Tumeenjoy mechi ya Ushindani mkubwa sana👏
2: Azam walikuja na Mifumo miwili iliyobadilika kwenye Transition. Bila mpira, walichagua kuanza mechi kwa kukabia juu 'High Line Pressing' ..Hapa uliiona 4-2-4 .. Yanga wakifanikiwa kwenye Build Up, Azam walirudi kwenye Flat 4-4-2 wakiubana uwanja katikati ya kiwanja
3: Yanga Mfumo ulibakia 4-2-3-1 lakini Utekelezaji ukabadilika. Hawakutaka kuuweka mpira kati kama kawaida yao. Walitega mashambulizi yao pembeni kwa kuutanua uwanja..
4: Nafikiri Tofauti unayoiona kwenye ubao wa Matokeo ni kutokana na QUALITY ya YANGA kwenye Baadhi ya Maeneo. Azam walihukumiwa hapo. Kivipi?
5: Nini Agrey angefanya zaidi? Alivuja jasho lake kwa asilimia zote Lakini Sekunde moja tu aliyomsahau MAYELE, Mpira ulikuwa kwenye neti zao. Ule ni Ubora wa viwango vya juu kabisa kwa MAYELE. TOP PLAYER. WHAT A GOAL!
6: Azam kama kuna Eneo ambalo wanatakiwa kuliboresha msimu ujao ni idara ya Golikipa.. Bado makosa binafsi ya magolikipa wao yamekuwa yakiwaadhibu kwenye michezo mikubwa! Kosa la AHMED SALULA ndio Lililowarejesha mapema mchezoni Yanga
7: DJUMA🙌 WOW! Kwa sekunde kadhaa alinikumbusha Ashley Young katika ubora wake!. Utulivu mkubwa, Krosi ya viwango.. Djuma ni kama alikuwa akiifanya kazi iliyokuwa ikiwapalia kina Ambundo
8: Mudathir Yahya🙌 WHAT A PERFOMANCE! wakati Yanga wakilaumu idadi ya pasi za Sure Boy zilizopotea, wasisahau Ubora wa Pressing ya Muda pale katikati ya kiwanja.. Kama Dube angekuwa kwenye ubora wake kwenye Kulink shambulizi, Muda angeweza kuondoka kiwanjani akiwa mshindi wa dimba.
9: Mechi zenye kasi ya juu hupima pia Level ya Utimamu wa mwili wa Waamuzi. Refa Nassoro Mwinchumu alizidiwa na kasi ya mchezo . Yako baadhi ya maamuzi aliyafanya bila uhakika kwa kuchelewa kufika kwenye matukio
10: NABI alishinda Mechi kwenye ile Sub ya kumuingiza MAKAMBO! Mabeki wa kati wa Azam ni kama hawakujiandaa kucheza dhidi ya washambuliaji wawili. Ile sub ndio ilikuja kumtoa Mayele kifungoni
Nb: Uteswe na Mafuta. Uteswe na Mpira.. Penda Yanga wewe😃
Post a Comment