Zuchu apokea tsh Mil. 100 na WCB




Msanii wa muziki kutoka lebo ya WCB @officialzuchu ameeleza furaha yake baada ya kupokea muamala wa tsh milioni 100 kutoka lebo ya WCB.

Muimbaji huyo ambaye ameshiriki kwenye EP ya Diamond kupitia wimbo ‘Mtasubiri’, hajaeleza pesa hizo zimetokana na nini.

“JUST A RANDOM THURSDAY AFU DON FUMBWE ANAKUTUMIA KA UJUMBE ZUCHU KUNA PESA YAKO IMEINGIA 🤔 CALLING MY BANKER IMEINGIA SH NGAPI ANAKWAMBIA 100MILLION 🤗 only in #WCB Rahaa”

Baada ya ujumbe huo, Rais wa lebo hiyo @diamondplatnumz , aliandika “WCB4LIFE”


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post