Zaidi ya tiketi 800,000 zauzwa mpaka sasa kwa Kombe la Dunia Qatar


 

Mashabiki wa kandanda wamenunua tiketi 804,186 za mechi za Kombe la Dunia nchini Qatar baadae mwaka huu katika awamu ya kwanza ya uuzajii. 

Shirikisho la kandanda Duniani na waandalizi wa kinyang'anyiro hicho FIFA wamesema wanunuzi wengiwa tiketi hizo wametokea Qatar, Marekani, England, Mexico, Umoja wa Falme za Kiarabu, Ujerumani, India, Brazil, Argentina na Saudi Arabia. 


Tiketi za mechi ya ufunguzi mnamo Novemba 21 -- ambayo itaihusisha wenyeji Qatar -- pamoja na fainali ya Desemba 18 ndizo zilizonunuliwa kwa wingi. 


Timu 32 zitashiriki tamasha hilo na mpaka sasa 27 tayari zimefuzu. Droo ya mwisho ya Kombe la Dunia ambapo timu zitapangwa katika makundi itafanyika Ijumaa Aprili mosi.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post