Wakenya Wenye Makasiriko "Mondi na Zuchu Wataachana tu"


TETESI za penzi la mastaa wawili wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na msanii wake, Zuchu zimewafikia baadhi ya Wakenya wenye makasiriko ambao wametamka waziwazi; “Wataachana tu

Hii ni baada ya gavana wa zamani wa Nairobi nchini humo, Mike Mbuvi Sonko ambaye ni maarufu kwenye mitandao ya kijamii kuposti video ya Diamond au Mondi na Zuchu wakiimba wimbo wao maarufu wa Mtasubiri kwa kupokezana na kudekeana kimahaba.
Katika video hiyo, Diamond na Zuchu wamekaa kwenye siti moja ya gari la kifahari aina ya Cadillac Escalade linalomilikiwa na jamaa huyo wakiimba Mtasubiri ambao ni miongoni mwa nyimbo kumi zinazopatikana kwenye albam fupi (EP) ya First Of All (FOA) ambayo Mondi ameachia hivi karibuni.

Hata hivyo, baadhi ya wafuasi wa Sonko wameipokea video hiyo kwa hisia tofauti ambapo baadhi yao ambao waliamini Diamond atamrudia dada yao, Tanasha Donna ndiyo wamepatwa na makasiriko na kuanza kuwaombea wawili hao dua mbaya wakisema;

“Wataachana tu!” Kwa miezi kadhaa sasa, Diamond na Zuchu wanasemekana ni wapenzi tangu siku ile ya Krismasi ambapo walinaswa kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar walipotoka ‘auti’ kwa mara ya kwanza kwa ajili ya chakula cha jioni.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post