Baada ya Msemaji wa Yanga Haji Manara kumteua Steve Nyerere kuwa Msemaji msaidizi wa klabu hiyo kutokana na kujiuzulu Usemaji wa Wasanii, Steve ameweka wazi kuwa sio kweli kwamba aliteuliwa, ilikuwa ni utani na dongo kutoka kwa Manara.
"Haji Manara ni Ndugu yangu mimi na yeye tuna historia kwenye Maisha yetu ya Upambanaji lakini kikubwa Tunataniana sana, Juzi Arusha Aliniwahi kunipa Dongo Hadharani katoa Ajira kwangu Nilifurahi sana Maana ucheshi unaongeza siku za kuishi".
"Ikumbukwe kuwa Haji Manara Ni MSEMAJI wa wananchi Timu kubwa katika ukanda wa Africa,...na kikubwa zaidi mimi ni shabiki wa Yanga kindaki ndaki."
"Ni Utani, sio kweli mimi MSEMAJI wa Yanga Ulikuwa utani tu kati ya mimi na Ndugu Yangu kaka yangu rafiki yangu.,..,kipenzi HAJI MANARA KING." - Steve Nyerere
Post a Comment