Shaffih Dauda "Itakuwa Jambo la Ajabu Kuzuia Dondo Cup"


“Mashindano yanayofanyika ya mitaani ni mashindano ambayo yamekuwepo miaka nenda rudi, naamini hata hata Rais Karia atakuwa amecheza kwa namna moja au nyingine siku moja kwenye makundi huko Tanga nyumbani alikokulia, kwa hiyo ni utamaduni ambao upo na sidhani kama unaweza kuzuiliwa na mtu yeyote kwamba mpira usichezwe. Na kama ikitokea hivyo itakuwa jambo la ajabu kwa sababu dunia nzima inapambana kupromoti mpira wa miguu uchezwe kwa namna yoyote ile, kwa nchi kama Tanzania sidhani kama hilo jambo linaweza likatokea kwa maana sasa badala ya ku-encourage na kutengeneza mifumo mizuri ya kuwapa nafasi vijana kucheza eti uje na wazo la kuzuia mashindano yasifanyike.

Nimesikia alichokuwa anazungumza Rais Karia, kwanza sijaona sehemu aliyozuia mashindano kufanyika, alikuwa na concern yake ya mashindano ya kufanyika kipindi cha msimu, akihisi kwamba yakifanyika wakati wa msimu wakati mashindano yanaendelea inaweza ikaleta mkanganyiko”

- @shaffihdauda


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post