Utafiti umegundua kwamba kuna idadi kubwa sana ya wanawake na wanaume wanao sumbuliwa na tatizo la kuwa na matumbo makubwa kiasi ama vitambi kwa lugha nyingine. Uchunguzi wetu umetuwezesha kubaini kuwa katika watu kumi wanao tembea bararani angalau watatu kati yao wanasumbuliwa na tatizo la kitambi.
Sababu kuu za tatizo la kitambi ni pamoja na;
Ulaji mbovu wa vyakula ( Ulaji usio zingatia mlo kamili ).
Ulaji mbovu wa vyakula unajumuisha ulaji wa vyakula vya aina moja kwa wingi kupita kiasi bila kuzingatia aina nyinginezo, mfano ulaji wa vyakula vya mafuta mafuta kwa wingi kupita kiasi.
Unywaji wa pombe kupita kiasi
Kutofanya mazoezi ya mwili na viungo pamoja na sababu nyinginezo.
Athari za tatizo la kitambi ni pamoja na :
Kuwa katika hatari ya kushambuliwa na magonjwa ya hatari kama vile kisukari, moyo na presha.
Kutokuwa na uwezo wa kumudu tendo la ndoa ( kwa wanaume )
Kupunguza mvuto wa kimapenzi ( kwa wanawake na hata wanaume pia )
Kupoteza fedha na muda mwingi katika kuhangaika kutafuta tiba ya tatizo pamoja na athari nyinginezo lukuki.
Post a Comment