Mwimbaji wa nyimbo za injili, msanii Ringtone Apoko toka Kenya ameingia kwenye headsline nchini humo baada ya kutoa orodha ya watu ambao anahisi ni wenye umri mdogo na wenye utajiri nchini Kenya.
Kama ilivyotarajiwa, amejiweka kwenye nafasi ya kwanza huku akiorodhesha mali yake kama vile nyumba tano za kifahari katika mitaa ya Runda, Karen na muthaiga. Pia ameeleza anamiliki hoteli na nyumba kadhaa za makazi, magari 7 aina ya Range Rover, Maybach, BMW n.k
Katika nafasi ya pili kupitia orodha hiyo ni mbunge wa eneo la Starehe Kaunti ya Nairobi, Charles Njagua Kanyi maarufu Jaguar, kwa mujibu wa Ringtone, Jaguar anamiliki nyumba mbili na magari matatu.
Kadhalika na hilo mkali huyo wa ngoma kama "Sisi ndio tuko", "Yesu Ang'are" na "Fagia" ameahidi kutoa orodha nyingine ya watu maarufu nchini Kenya ambao amesema ni wapiga kelele ilhali hawamiliki chochote.
Post a Comment